Karibu Ukurasa Wetu Wa Kiswahili

Itambue na Kuitawala Nafsi Yako: Mwili, Akili na Roho.

Maadili Leadership Solutions inakupa taaluma, mbinu na nyenzo za jinsi ya kuitambua, kuitibu na kuimudu nafsi ili uweze kufkia mafanikio na kuyafurahia maisha.

Ifahamu Nafsi: Mwili, Akili na Roho

Katika Programu yetu ya Mtindo wa Maisha ya Ayurveda, utaweza kuitambua nafsi yako na kupitia dodoso letu la Dosha, utajibu maswali yatakayo kufanya utambue talanta ulizorithi kutoka kwa wazazi wako na vizazi vyao vyote tangu siku ile wewe ulivyotungwa kama mimba. Utajifunza namna ya kupangilia maisha yako ya kila siku kwa kila majira yanavyobadilika ili uweze kuishi maisha mema.

Kuwa na Uhuru Wa Mihemko

Fahamu jinsi ya kuwa na uhuru na amani ndani yako na wote unaoishi nao kaitika jamii, familia na mahali pa kazi. Mafundisho haya yatakuwezesha kuzikubali hisia zako kaitka mwili huku ukiusikiliza, kuutafakari na kuzifanyia kazi jumbe ziletwazo na hisia zako.

Chakula Kama Tiba ya Mwili, Akili na Roho

Lishe Bora ni msingi kwa uhai wako, afya na maisha marefu. Ni muhimu kula chakula kwa Uwiano sawia wa Akili na Mwili. Programu yetu itakufundisha umuhimu wa kuimarisha mmeng’enyo sahihi kwa afya na jinsi ya kuepuka mmeng’enyo usiofaa ambao husababisha sumu. Pia utafahamu umuhimu wa ladha sita za vyakula pamoja na siri iliyopo kwenye mlo wenye rangi nyingi.

Tiba Iliyo Ndani Mwako.

Fahamu jinsi milango mitano ya utambuzi inavyoweza kukufanya ufurahie ulimwengu ulivyo. Utajifunza jinsi ambavyo sauti, hisia, ladha na harufu vinavyoweza kuleta uwiano bora. Kupitia mafunzo yetu uatapata mbinu mbalimbali za tiba kupitia sauti, tiba kupitia kuona, tibakupitia ladha, harufu, kucheka, tafakari mchakato pamoja na Yoga.

Jipatie Kitabu

aFYA tIMAMU

Kitabu cha AFYA TIMAMU kinatoa muongozo wa Programu ya Mtindo wa Maisha ya Ayurvedic Iliyoandaliwa na Kituo cha Chopra. Ndani ya kitabu hiki utapata taaluma, nyenzo na mbinu za jinsi ya kuitambua, kuitibu na kuimudu nafsi yaani Mwili, Akili na Roho. Kitabu hiki hakiuzwi bali kinapatiwa kwa yule ambaye atajiunga na programu zetu za mafunzo. 

Jipime na Dodoso la Dosha

Maswali ya dodoso la Dosha kutathmini maisha yako ya sasa
pamoja na changamoto za karibuni, maradhi au mabadiliko mengine katika maisha yako. Ukijibu maswali haya utaweza kupata taarifa kuhusu hali yako halisi ya maisha ya utotoni na jinsi gani yameathiri maisha yako ya sasa.